Mgombea aliyetabiriwa kifo kumbe ni Mtikila

MTABIRI maarufu nchini, Maalim Hassan Yahya Hussein, amesema utabiri wake alioutoa mwaka 2014 kwamba mgombea urais mmoja atafariki dunia ghafla kabla ya uchaguzi, umetimia baada ya kifo cha Mchungaji Christopher Mtikila na kuwaacha salama wagombea Edward Lowassa na Dk. John Magufuli.

Maalim Hassan aliyasema hayo alipozungumza na gazeti la Uwazi juzi ambapo alisisitiza kuwa utabiri wake alioutoa Desemba 28, 2014 katika mkutano wake na waandishi wa habari ofisini kwake, haukumlenga mtu.

Mchungaji Mtikila ambaye alikuwa akigombea urais kupitia Democratic Party (DP) kabla ya kuenguliwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec), alifariki dunia Oktoba 4, 2015 kwa ajali ya gari kijijini Msolwa, Chalinze, mkoani Pwani akitokea Njombe.

“Nilipoutoa utabiri ule mengi yalisema na watu wakawataja wagombea fulani, lakini niliwaambia kwamba utabiri haulengi mtu na sasa umempata Mchungaji Mtikila.

“Mtikila alikuwa mgombea urais,  alichukua fomu na watu wakaona akiwa na mkoba kama wa wagombea wenzake, akakataliwa na tume lakini akakata rufaa… angeweza pia kushinda rufaa yake,” alisema Maalim Hassan.

Aliongeza kuwa, mara baada ya utabiri wake alipigiwa simu na makada wa vyama viwili – Chama cha Mapinduzi (CCM) waliodai kuwa mgombea wao Dk.  Magufuli haumhusu na wale wa Chadema nao wakasema mgombea wao,  Lowassa hawezi kuchuliwa hivyo – akawajibu wote kwamba utabiri wake haumlengi mtu.

“Niwahakikishie wananchi kwamba, kinyota wagombea wote wa urais waliobaki sasa wako salama na watashiriki kuchagua viongozi Oktoba 25, mwaka huu,” alisema Maalim Hassan.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo