MWENYEKITI wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Damian Lubuva hivi punde amesema kufutwa kwa uchaguzi wa Zanzibar hakutasababisha kuahirishwa au kufutwa kwa uchaguzi wa Tanzania Bara na kusisitiza kuwa mchakato wa uchaguzi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania unaendelea kama ulivyopangwa.
Jaji Lubuva ameongeza kuwa tayari NEC imepokea taarifa zote za matokeo ya urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutoka Zanzibar na hayakuwa na kasoro.
Aidha, Lubuva ameongeza kuwa uchaguzi wa Zanzibar unasimamiwa na Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) na uchaguzi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania unasimamiwa na NEC ambazo zina katiba mbili tofauti.