Mbunge wa jimbo la Ludewa, Deo Filikunjombe na Capt. William Silaa (baba yake Jerry Slaa), wamethibitika kupoteza maisha kwa ajali ya helkopta katika eneo la Msolwa, hifadhi ya Selous.
Deo anakuwa mbunge wa sita kupoteza maisha katika kipindi hiki cha Uchaguzi Mkuu.
Jerry Slaa, ameandika ujumbe kwenye Instagram kuhusu msiba huo uliolifika taifa.
“Kwa masikitiko makubwa nimepokea taarifa rasmi kutoka kwa timu ya uokoaji imefanikiwa kufika eneo la ajiali na kukuta abiria wote na rubani wamepoteza maisha.
"Nimempoteza Baba na rubani mzuri wa nchi yetu Capt.William Silaa,nimepoteza rafiki na kiongozi wangu Mhe.Deo Filikunjombe. Nawapa pole wote waliopoteza ndugu zao. Nawaombea marehemu mapumziko ya Amani.
"Nawashukuru wote walioshirikiana na familia kusaidia uokozi.
Namshukuru Mhe.Rais Jakaya M Kikwete, Dr.John Pombe Magufuli, IGP Ernest Mangu, Katibu Mkuu MU Dr.Meru, Kampuni ya Everest Aviation ,Wabunge, MaDC, Maafisa wa TCAA na wote walioshiriki kuwatafuta wahanga wa tukio hili.
"Tutajuzana taarifa na mipango mingine.”
Naye mjumbe wa kamati ya kampeni ya CCM, ambaye pia ni Naibu Waziri wa Wizara ya Sayansi, Teknolojia na Mawasiliano, January Makamba ametweet kuhusu taarifa hizo.
Nimetoka kupokea taarifa inayothibitisha kwamba chopa aliyokuwa amekodi Ndugu yetu Filikunjombe imeanguka na watu wote wamefariki.
— January Makamba (@JMakamba) October 16, 2015
Siku mbili zilizopita niliongea kwa kirefu na Deo kuhusu mikakati. Nimepoteza rafiki na ndugu. Mungu amrehemu na pole kwa familia za wafiwa.
— January Makamba (@JMakamba) October 16, 2015