Mgombea urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) John Magufuli, leo alimwaga sera katika Wilaya ya Bahi mkoani Dodoma na kuingia Mkoa wa Singida ambapo alifanya mikutano kwenye vijiji miji ya Chikuyu, Kilimatinde, Manyoni, Itigi, na kumalizia na Itigi iliyopo Jimbo la Singida Mashariki.
Katika mikutano hiyo Magufuli aliitangaza ilani ya utekelezaji ya chama chake ambayo inatoa kipaumbele kwa mambo kadhaa ikiwemo kupunguza shida ya maji safi na salama, huduma za afya, barabara, kupunguza ushuru kwa wafanyabiashara wadogowadogo na wakubwa, kutoa mikopo kwa ajili ya mitaji, elimu bure na mengine mengi.
Akimwaga sera hizo Magufuli alitoa ufafanuzi wa jinsi atakavyoiteleza ilani hiyo hali iliyosababisha kila alitoa ufafanuzi watu wamshangilie kwa vifijo na nderemo.
