Kauli ya kuumiza kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM)

Jioni ya jana, Oktoba 15, helikopta namba 5Y-DKK ilipata ajali katika eneo lisilofikika kirahisi (remote) la mbuga ya wanyama ya Selous, ikitokea Dar Es Salaam kwenda Ludewa. Vyombo vya serikali (Wizara ya Maliasili na Utalii, TCAA, Polisi) pamoja na kampuni binafsi za usafiri wa anga wameshirikiana usiku kucha kufika eneo hilo. Katika ajali hii Ndugu Deo Haule Filikunjombe (Mbunge wa Ludewa) na Kapteni William Silaa pamoja na watu wengine wawili wamefariki dunia. Chama na nchi imepoteza kijana makini, kiongozi bora, tegemeo la wana Ludewa na mfano imara kwa vijana wa Tanzania. Familia ya Kapteni William Silaa imepoteza baba, nchi imepoteza rubani mzuri. Tunaungana na familia zote katika kipindi hiki kigumu.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright 2025 EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo