Jaji Mkuu ageuka "mbogo" ni baada ya kunukuliwa kuunga mkono kukaa mita 200

2.0 Taarifa hii si ya ukweli na ni ya upotoshaji,Mhe Jaji Mkuu hajawahi kuzungumzia chochote kuhusu sheria hiyo ukitilia maanani kesi hiyo iko Mahakama Kuu shauri Namba 37 ya 2015 iliyofunguliwa na Bi. Amy Kibatala dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) na Mkurugenzi wa Uchaguzi (DE) na itatolewa maamuzi kati ya tarehe 22 au 23 mwezi huu. Hivyo, kwa mujibu wa sheria Mhe.Jaji Mkuu asingeweza kuzungumzia chochote kuhusu sheria hiyo kwa kuwa suala hilo likoMAHAKAMANI.      
                                                                          
3.0 Tulimwandikia Mkurugenzi wa Habari MAELEZO nakala East Africa Television na kufuatilia kwenye Baraza la Habari (Media Council) kuomba maelezo ya kina na usahihi wa taarifa hiyo,  tarehe 21/10/2015 tumepokea barua Kumb Na EATV/ADMN/096/10/2015 ilyosaniwa na Bi Regina Mengi Mkurugenzi Mtendaji wa East Africa Television akiomba msamaha kuhusu taarifa hiyo potofu na kuwa watatoa maelezo ya ziada kuwa, taarifa hiyo haikutolewa na Mhe.Jaji Mkuu wa Tanzania
 
Tunashukuru kwa ushirikiano mkubwa tulioupata toka uongozi wa juu kabisa wa East Africa Television kwa kuomba radhi mapema na Tunamini kuwa, vyombo vya Habari na Wananchi kwa ujumla vitasitisha usambazaji wa taarifa hii iliyokuwa si sahihi.
                                                                                                                                 
Barua ya kuomba radhi imeambatanishwa:

 Imetolewa na:                    
MTENDAJI MKUU WA MAHAKAMA                   


MAHAKAMA YA TANZANIA


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo