
Ni kauli ya mgombea urais wa chama cha mapinduzi CCM Dr John Pombe Magufuli inayoashiria kutaka uwajibikaji na uadilifu katika kuwatumikia watanzania ili nchi iweze kupaa kimaendeleo na kupunguza kiwango cha umasikini kwa watanzania kwa kutumia rasilimali zilizopo na kuahidi kuifanya Bagamoyo kuwa kitovu cha uwekezaji.
Katika kuhakikisha serikali yake inawajibika kwa watanzania wote na kila mmoja kupata haki yake kwa mujibu wa sheria za nchi Dr Magufuli anawahakikishia kulipwa fidia stahiki kwa wakazi wa Bagamoyo ambao ardhi yao ilitwaliwa kupisha eneo la uwekezaji la EPZD.
Akitokea wilayani Same mkoani Kilimanjaro kuelekea Bagamoyo mkoani Pwani ambapo haikuwa rahisi kufika katika mikutano rasmi ya kampeni kutokana na kusimamishwa mara kwa mara barabarani na wananchi waliokuwa na kiu ya kutaka kumuona na kumsikia alipowasili Bagamoyo, Dr Magufuli ameonesha kukerwa na tatizo la ukosefu wa maji.
Katika mji wa Bagamoyo na kuahidi kulipatia ufumbuzi wa haraka pindi atakapoingia madarakani.