Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Geita kimesema kimejipanga kutumia askari wasiovaa sare ambao watakaa maeneo tofauti wakipima mwendo kasi wa madereva na kuwachukulia hatua ili kudhibiti mwendo kasi ambao kwa kiasi kikubwa ndiyo chanzo cha ajali.
Katika kipindi cha Januari hadi Septemba mwaka huu, jumla ya matukio 76 ya ajali wametokea nyingi zikionyesha ni uzembe wa madereva kwa kutozingatia sheria za usalama barabarani na kusababisha ajali zinazoepukika.
Suala la ajali limekuwa ni tatizo sugu linalosababisha madhara ya kifo na ulemavu kwa jamii Kwa mwaka huu kuanzia januari hadi septemba ajali 76 zilizotokea zimesababisha majeruhi 19 na idadi ya watu waliokufa ni 61.
Ongezeko la kubwa la watumiaji wa barabara hasa wapanda baiskeli na pikipiki wanaosababisha msongamano mkubwa unaoongeza uwezekano wa ajali kutokea.
Akizungumza katika mkutano wa kuhamasisha matumizi salama ya barabara Kamanda wa usalama barabarani Mkoa Patrick Hussein amesema madereva wengi wamekuwa wakipeana ishara wanapoona askari wa barabarani na hivyo kutembea kwa mwendo mdogo katika maeneo yenye askari.
Elimu kila mara hutolewa kwa watumiajai wa barabara na watu kutakiwa kuheshimu alama za barabarani.
Mkuu wa Mkoa wa Geita Fatma Mwassa amekemea vikali juu ya baadhi ya matrafki wanaopewa rushwa na kutoa leseni kinyume na taratibu kwa mtu asiyefuzu mafunzo ya udereva.
Pamoja na hayo kikosi cha usalama barabarani kinakabiliwa na changamoto ya wizi wa vyuma vya usalama barabrani,ubovu wa miundombinu unaosababisha ajali na baadhi ya maeneo kufutika alama za barabarani.