Watafiti wanaoandaliwa kufanya utafiti wa masuala mbalimbali hasa ya kielimu kwa watoto wilayani Makete mkoani Njombe wametakiwa kufanya kazi hiyo kwa moyo mkunjufu, na si kupika takwimu kwa maana ya kutoa takwimu za uongo
Kauli hiyo imetolewa leo na Afisa elimu Msingi wilaya ya Makete Mwl. Antony Mpiluka (pichani juu) wakati akifungua mafunzo ya siku mbili kwa watafiti wanaotarajiwa kuendesha zoezi hilo wilayani hapa, mafunzo yanayotolewa na shirika lisilo la kiserikali la SUMASESU
Mpiluka amesema kutoa takwimu za uongo kutapelekea madhara makubwa kwa wilaya huku akitolea mfano kipengele cha watoto kujua kusoma kiswahili na kiingereza pamoja na kufanya hesabu, kuwa endapo watapika takwimu na kuonesha watoto wanajua kusoma wote ili hali hawajui, itapelekea wilaya kuwa na sifa nzuri lakini ni ya uongo
Mafunzo hayo ni ya siku mbili na yameshirikisha vijana kutoka kata mbalimbali za wilaya ya Makete na yataendeshwa kwa siku mbili
Baadhi ya washiriki wakifuatilia