Vitendo vya Wanawake kufanya biashara ya kujiuza sio story ngeni kukutana nayo, nchi zimekuwa na maamuzi tofauti kuhusu kesi ya Wanawake wanaofanya Biashara hiyo, Ujerumani hiyo ni biashara halali na kuna maeneo maalum kabisa yametengwa kwa ajili ya kufanya hizo shughuli !!
Nakuunganisha na Story kutoka Nigeria, Wanawake 30 wamekamatwa na kufikishwa Mahakamani kwa kosa la kukutwa wakifanya Biashara haramu ya kujiuza… Mahakama ya Hakimu Mkazi Jiji la Lagos imewahukumu wanawake hao kifungo cha wiki sita jela kwa kosa hilo.
Mahakama hiyo ilitoa adhabu hiyo ya hukumu au Watuhumiwa hao walitakiwa kulipa faini ya Naira 10,000 ili waepukane na adhabu ya kifungo… Naira 10, 000 ni kama Tshs. 108,000/=.