Sikutatu baada ya makanisa matatu ya madhehebu ya dini ya kikristo kuchomwa na kuteketea kwa moto na watu wasiojulikana mjini bukoba jeshi la Polis mkoani Kagera linawashikiria watu saba wanaodaiwa kuhusika katika kuchoma makanisa hayo.
Akiongea mjini bukoba kamanda wa jeshi la Polisi mkoani Kagera Augustine Ollomi amesema matukio hayo yameleta taharuki kwa waumini wa makanisa hayo,majirani na wapenda amani wote wa ndani na nnje ya mkoa wa Kagera na kuongeza kuwa jeshi la Polisi mkoani hapo limeunda timu maalumu ya wapelelezi kuchunguza kwa kina chanzo cha matukio hayo ambayo yanaweza kusababisha viashiria vya uvunjifu wa amani katika mkoa huo.
Mkuu wa mkoa wa Kagera John Mongera akizungumza mara baada ya kutembela makanisa hayo na kujionea maafa yaliyotokea nakusema kuwa serikali kwa kutumia jeshi la Polisi itahakikisha inabaini watu waliohusika katika kufanya tukio hilo wanakamatwa nakufikishwa mahakamani ambapo pia amewaomba wananchi kutoa ushirikiano kwa jeshi la la polisi katika kufanya upelelezi wa haraka kwalengo kubaini wahusika walioshiriki kufanya tukio hilo.
Wakizungumza kwa masikitiko makubwa baadhi ya wa chungaji wamesema endapo serikali ipotialia mkazo katika kudhibiti tatizo hilo watalazimika kufanya maandamano kwalengo la kupiga vitendo viovu vinavyo fanywa na baadhi ya watu wasiomjua mungu ikiwa ninjia mojawapo ya kuishinikiza serikali kuhakikisha vitendo vya ainahiyo vinakomeshwa.
Makanisa yalioteketezwa kwa moto hivi karibuni na watu wasiojulikana nikanisa la pentekoste Assembres Of God(PAG)lililopo eneo la Buyekera Halisi,kanisa la Living Water Intanational lililopo mtaa wa mtoni kata ya Bukoba manispaa ambalo lilikuwa kiongozwa na mchungaji Vedasto Athanas,na kanisa la Evengelical Assebles Of God lililopo eneo la Omkibeta ambalo lilikuwa liongozwa na mchungaji alistides Kabonaki yote yalichomwa na kutekektea kwa moto kwa sikumoja.