Abiria waliokuwa wakisafiri na basi la OTA High Class kutoka jijini Dar es Salaam kuelekea mkoani Njombe wamenusurika kufa baada ya basi hilo kupata ajali ya kugongana na gari Dogo eneo la TFA mita chache kabla ya kufika kituo kikuu cha mabasi mkoani hapo
Ajali hiyo imetokea leo saa 12 jioni baada ya basi hilo kugongana na gari dogo aina ya probox, hata hivyo hatujapata taarifa zaidi za madhara kwa waliokuwa kwenye gari dogo