Mtumbwi wazama Ziwa Viktoria na kuua wavuvi haramu

Watuhumiwa watatu wa uvuvi haramu wamekufa baada ya mtumbwi waliokuwa wakisafiria kuzama katika Ziwa Victoria wakati wakipelekwa kituo cha polisi na askari waliowakamata.
Katika tukio hilo, bunduki ya kivita aina ya AK-47 yenye namba 30900 pia ilizama ziwani na askari wa kikosi maalum cha wapiga mbizi kutoka kitengo cha Marine na Bandari kulazimika kufanya kazi ya ziada kuiopoa majini.
Ajali hiyo ilitokea juzi baada ya mtumbwi huo kupigwa na dhoruba kali.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Joseph Konyo, alithibitisha tukio hilo lilitokea Agosti 18, mwaka huu, wakati askari hao walipokuwa wakisafiri na watuhumiwa hao katika mtumbwi uliozama wakati wakiwapeleka Kituo cha Polisi Kageye.
Aliwataja waliokufa katika tukio hilo kuwa ni, Dioniz Masatu (26), Revocatus William (26) na Stadius Audaxi (23), wote wakazi wa kjiji cha Kazilatemwa, wilayani Muleba na walionusurika ni Shabaan Maiga (45) na Fikiri Mafulu (46) ambao walijiokoa kwa kuogelea.
Kamanda Konyo alisema askari mmoja wa hifadhi aliogelea umbali wa zaidi ya mita 800 na kujiokoa, huku mwingine akishikilia mtumbwi uliopinduka na baadaye kuokolewa kabla haujazama.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo