Mgombea mwenza wa urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu, ameonya vijana waendesha bodaboda kuacha tabia ya kuwarubuni wanafunzi wa kike kwa chipsi na 'lifti' jambo linalowasababishia mimba zisizotarajiwa.
"Vijana ninyi na vipikipiki vyenu mnawaharibia maisha watoto wa kike kwa kuwapa mimba zisizotarajiwa," alisema Samia
Kutokana na tatizo hilo, Samia alisema akichaguliwa yeye na mgombea wa urais kupitia CCM, Dk. John Magufuli atahakikisha anakabiliana na hali hiyo kwa kujenga mabweni ya wasichana katika shule za kata.
Alisema bila mabweni wasichana wa kike wataendelea kupata mimba zisizotarajiwa na hivyo kuharibu maisha yao.
