Madereva mkoani Njombe waelezea manyanyaso wanayoyapata barabarani


Na Gabriel Kilamlya Njombe

Wakati Jeshi la Polisi Mkoani Njombe Likihitimisha Kilele Cha Wiki ya Nenda Kwa Usalama Barabarani Baadhi ya Madereva Mkoani Hapa Wamelalamikia Manyanyaso Ambayo Wamekuwa Wakiyapata Wakiwa Barabarani.

Wakizumgumza Katika Maadhimisho Hayo Yaliyofanyika Katika Viwanja Vya Shule ya Msingi ya Mtakatifu Bakita Mjini Njombe Baadhi ya Madereva wa Daladala na Boda Boda Wamesema Kuwa Wamekuwa Wakipata Manyanyaso ya Kuombwa Rushwa Hata Kama Hawana Kosa Lolote Wakitumia Lugha za Jiongeze au Ya Maji.

Aidha Wamesema Kuwa Bado Serikali Kupitia Wakala wa Barabara TANROAD Mkoa wa Njombe Wanapaswa Kuangalia Namna ya Kuongeza Vituo Vya Abiria Kutokana na Umbali wa Kutoka Kituo Kimoja Kwenda Kingine.

Taarifa ya Jeshi la Polisi Mkoa wa Njombe Kitengo Cha Usalama Barabarani Iliyosomwa na Kamanda wa Kikosi Hicho Mkoa wa Njombe Kelvin Ndimbo Imeeleza Kuwepo Kwa Ongezeko la Maduhuri Kupitia Makusanyo ya Faini za Makosa Mbalimbali Jambo Ambalo Linaonesha Kuwepo Kwa Ongezeko la 
Makosa Barabarani.

Kwa Upande Wake Mgeni Rasmi Katika Maadhimisho Hayo Ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Njombe na Mkuu wa Mkoa Huu Dokta Rehema Nchimbi Amelaani Vitendo Vya Rushwa Vinavyotajwa Kufanywa na Baadhi ya Askari wa Usalama Barabarani na Kwamba Kinachotakiwa Kamanda wa Polisi Mkoa Aanzishe Miradi Itakayowasaidia Askari Hao Kuepukana na Rushwa.

Pamoja na Mambo Mengine Lakini Pia  Amesema Kuwa Ajali za Barabarani Zinaweza Kuepukika Kabisa Endapo Askari Watakuwa Makini na Kazi Yao Barabarani Kwa Kujiepusha na Rushwa Ikiwa ni Pamoja na Ukali Kwa Wanaokiuka Sheria za Barabarani.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo