Kagera wampigia magoti mgombea urais wa CCM Dkt Magufuli

Wananchi wa mkoa wa Kagera na viunga vyake wamemuomba mgombea wa kiti cha urais kupitia CCM Dr John Pombe Magufuli kuimarisha bei ya zao la kahawa ili waweze kuinuka kiuchumi kutokana na zao hilo kuwategemeo la kibiashara kwa wakazi hao sambamba na kuboresha usafiri wa majini katika ziwa Victoria. 

Kauli hiyo ya Dr John Pombe Magufuli inaakisi vilio vya watanzania hasa wanyonge ambao wengi wao ni wakulima na wafugaji ambapo baadhi ya wakazi wa Bukoba mkoani Kagera wanawasilisha kilio chao kuhusu bei ya zao la Kahawa na usafiri wa majini hususani katka ziwa Victoria. 
 
Dr John Pombe Mgufuli ambaye hii leo amefanya mikutano ya kampeni katika maeneo ya Muleba, Nshamba, Kamachumu, Kemondo, Bukoba vijijini na hatimae Bukoba mjini amewaambia wakazi wa mkoa huo kuwa baada ya serikali kuimarisha mtandao wa barabara kutoka Bukoba hadi Dar es Salaam na nchi jirani, awamu ya tano imejipanga kuimarisha usafiri katika ziwa Victoria ambapo meli mbili zitanunuliwa.
 
kuhusu kilio cha kuimarisha bei ya zao la Kahawa Dr Magufuli anaelezea mikakati aliyo nayo kuimarisha bei ya zao hilo ili liendelee kuwa zao kuu la biasahara na kuwanufaisha wakazi wa mkoa wa Kagera.
 
Aidha Dr Magufuli ameonesha kushangazwa na kauli zinazotolewa na waliokuwa viongozi waandamizi wa serikali kuwa serikali haijafanya lolote na kuongeza kuwa viongozi hao wanapaswa kuwaomba radhi watanzania.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo