Dr. Magufuli leo pia amefanya mikutano kadhaa ya kampeni mkoani Iringa ambako alilazimika kumalizia viporo hivyo vilivyokuwa vimebaki mkoani humo. 

Wananchi kwa maelfu wakimsikiliza Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia huko Makambako mkoani Iringa ambako alipita leo kumalizia viporo vya mkoa huo kwenye kampeni zake.


Wagombea wa nafasi mbalimbali wa Mafinga wali-Magufulika mbele ya Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM Dkt. John Pombe Magufuli katika jimbo la Mafinga mkoani Iringa ambako alipita leo kumalizia viporo vya mkoa huo kwenye kampeni zake.

Mgombe ubunge jimbo la Mafinga Mjini kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Cosato Chumi, aki-Magufuli-ka

Mgombea Ubunge Jimbo la Mufindi Kaskazini, Mahamudu Mgimwa akidhihirisha kuwa yupo fiti.
![]() |
| Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia gharika ya wananchi wa Makambako mkoani Iringa ambako alipita leo kumalizia viporo vya mkoa huo kwenye kampeni zake. |
