Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
ALIYEKUWA Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Shinyanga, Hamis Mgeja ameng'atuka uanachama wa CCM pamoja kujiuzulu nafasi ya Uenyekiti wa chama hicho.
Akizungumza na waandishi wa habari leo katika Ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo jijini Dar es Salaam,Mgeja amesema kuwa ametafakari sana na kuona aungane na chama hicho.
Mgeja amesema kuwa anaondoka kwenda kutafuta mabadiliko katika Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na kuongeza kuwa wametumikia chama hicho kwa muda mrefu lakini sasa imefika wakati wa kuondoka.
Aidha amesema kuwa CCM ya sasa imekuwa na vitu ambavyo vinafanywa na watu baadaye kuikigharimu chama kutokana na kuacha msingi wa kukubali maoni ya wanachama.
Wakati huo huo katika mkutano huo aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam,John Guninita naye ameng'atuka katika chama hicho na kujiunga na Chadema kuongeza nguvu Ukawa.
Guninita amesema kuwa sasa umefika wakati wa kuondoka kutokana na Chama kuacha kusikiliza wanachama wake na badala yake kuendeleza chuki ndani ya Chama.
Aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM, Mkoa wa Shinyanga, Hamis Mgeja akizungumza na waandishi wa (habari hawapo pichani )juu ya kung'atuka katika chama hicho na kujiunga na Chadema leo katika ukumbi wa Idara ya habari Maelezo jijini Dar es Salaam, Kulia ni John Gudinita.
Aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM, Mkoa wa Dar es Salaam, John Gudinita akitangaza kujiuzulu katika chama hicho na Kujiunga na Chadema leo majira ya saa tano katika ukumbi wa Idara ya habari Maelezo jijini Dar es Salaam. kushoto Sheik Rajab Katimba na kulia ni Aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM, Mkoa wa Shinyanga, Hamis Mgeja.
AliyekuwaMwenyekiti wa CCM, Mkoa wa Shinyanga,Hamis Mgeja akionesha kuwa yeye ni chadema kwa sasa.
Waandishi wa habari wakimsikiliza Mwenyekiti wa CCM,Mkoa wa Shinyanga,Hamis Mgeja wakati akitangaza kujiuzulu katika chama hicho na Kujiunga na Chadema leo majira ya saa tano katika ukumbi wa Idara ya habari Maelezo jijini Dar es Salaam.
(Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii)