Wananchi watoa kichapo kwa mtu aliyechoma matairi 400 kwenye makazi ya watu

Katika hali isiokuwa ya kawaida  mfanyabishara mmoja  amejikuta akiambulia kichapo kutoka kwa wananchi wenye hasira kali  baada ya kuchoma matairi zaidi ya 400 katikati ya makazi ya wananchi katika kijiji cha Kilimahewa kata ya Mbuyuni manispaa kwa lengo la kutaka kupata mabaki ya nyaya ili kuuza kama chuma chakavu.

Mtu huyo aliyejulikana kwa majina ya Mosha Ramadhani amejikuta akiwa mikononi mwa kamati ya ulinzi na usalama ya kijiji baada ya kupata kichapo ambapo amekiri  kufanya makosa ya kuchoma matairi katika makazi ya watu kwa nguvu  baada ya kukatazwa na wananchi  kwa kisingizio cha hali ngumu ya maisha na alifanya hivyo ili kupata nyaya za kuuza aendeshe maisha. 
 
Kwa upande wao wananchi wa kijiji cha kilima hewa akiwemo mwenyekiti wa kijiji hicho Sajigwa Mwakiruma wamelaani  kitendo hicho ikiwa ni pamoja na mwenyekiti  walichukua hatua  kumpeleka mtuhumiwa  katika kituo cha polisi kwa tuhuma za kuharibu mazingira.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo