Wafugaji 300 Monduli wachoma moto kadi za CCM na kujiunga CHADEMA

Zaidi ya wanachama mia tatu wa CCM kutoka jamii ya kifugaji katika kata ya Engaruka wilaya ya Monduli wamerudisha kadi za CCM na  kujiunga na chadema huku wakidai maamuzi yao yametokana na  utashi wao binafsi kwa kuzingatia hali halisi ya kisiasa ilivyo hivi sasa.

Blog hii ilifika katika kijiji cha Engaruka na kushuhudia mamia ya wanachama waliyo kusanyika katika mkutano wa hadhara kukusanya kadi za CCM kuzichoma moto  na kuchukua kadi za CHADEMA huku wakiainisha sababu zilizo fanya kufikia maamuzi hayo.
 
Akizungumza baada ya kuwapokea wanachama hao  akiwemo mwenyekiti wa kijiji cha Engaruka Lewanga Kivuyo mwenyekiti wa Bavicha wilaya ya Monduli Yasini Shabani amesema Chadema ni chama kinacho zingatia haki ya kila binadamu na kila mwanachama.
 
Kada maarufu wa chadema Julias Karanga amewataka wananchi kuwa wavumilivu kwakuwa mabadiliko yana changamoto nyingi za kukatisha tamaa kutoka kwa mahasimu lakini kwa nguvu ya mungu watayashinda.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo