Idadi ya vyama vya siasa vitakavyoshiriki uchaguzi mkuu mwaka huu 2015


VYAMA vya siasa vinavyotakiwa kushiriki kwenye Uchaguzi Mkuu mwaka huu baadaye Oktoba 25 mwaka huu ni 22.

Taarifa iliyotolewa na Msajili wa Vyama vya Siasa jana Dar es Salaam na kusainiwa na Msajili Msaidizi, Sisty Nyahoza, imetaja idadi hiyo ya vyama vyama hivyo, ambavyo ni vyenye usajili wa kudumu kuwa ni ni Chama Cha Mapinduzi (CCM), Chama cha Wananchi (CUF), Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Union for Multiparty Democracy (UMD) na Chama cha NCCR-Mageuzi.

Vingine ni National League for Democracy (NLD), United Peoples’ Democratic Party (UPDP), National Reconstruction Alliance (NRA), African Democratic Alliance Party (TADEA), Tanzania Labour Party (TLP) na United Democratic Party (UDP).

Vyama vingine ni Demokrasia Makini (Makini), Chama cha Haki na Ustawi (Chausta), Democratic Party (DP), African Progressive Party of Tanzania (APPT-Maendeleo) na Jahazi Asilia.

Vile vile kuna chama cha Sauti ya Umma (SAU), Tanzania Farmers Party (AFP), Chama cha Kijamii (CCK), Alliance for Democratic Change (ADC), Chama cha Ukombozi wa Umma (Chaumma) na Alliance for Change and Transparency (ACT-Wazalendo).


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo