Viongozi na wanachama 11 wa ACT Wazalendo wahamia CHADEMA

Viongozi wandamizi na wanachama wa chama cha Allience for Change and Transparency ACT mkoa wa Morogoro akiwemo mwenyekiti wa chama hicho mkoa Bwana Magnus Msambira wameamua kukihama chama hicho na kujiunga na chama cha demokrasia na maendeleo Chadema.

Akizungumza mara baada ya kukabidhi  kadi ya chama hicho na kupokea kadi ya Chadema mwenyekiti wa ACT mkoa wa Morogoro Magnus Msambira amesema aliamini ACT ni chama kinachosimamia misingi kumi lakini cha kushangaza viongozi wa ACT wa taifa ndio wamekuwa wa kwanza kuvunja misingi hiyo kwa kuwapora wanachama wake mamlaka na uwezo wa kuchagua viongozi wanaowataka.
 
Naye mgombea ubunge jimbo la mlimba wilaya ya Kilombero Susan Kiwanga pamoja na mengine amesema jimbo hilo linakabiliwa na matatizo ya ardhi, kero za walimu, wafanyakazi wa Tazara pamoja na migogoro ya ardhi ambapo ameitaka tume ya uchaguzi kuongeza vituo vya wananchi kuhakiki majina yao katika daftari la kudumu la wapigakura ili wawe na uhakika wa kuchagua viongozi watakaowaletea maendeleo.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo