Umeipata hii mpya ya Kafulila kuhusu usaliti wa Dkt Slaa

Mbunge wa Kigoma Kusini anaye maliza muda wake, David Kafulila amefunguka na kusema anaamini Katibu Mkuu wa chama cha Chadema Dk. Willibrod Slaa hawezi kuwasaliti watanzania wakati huu wa ukombozi wa pili.

Akichat Live kupitia ukurasa wa facebook wa EATV katika kipengele cha Kikaangoni, Kafulila amesema Dk. Slaa bado kampumzika na anaendelea kutafakari, ingawa kwa mtazamo wake anaamini hatawaangusha watanzania katika ukombozi huu wa pili.
"Dk. Slaa bado kapumzika, anaendelea kutafakari. Naamini hatawaangusha watanzania katika ukombozi huu wa pili. pengine tumpe muda tu, " alisisitiza Kafulila katika moja ya posti yake.
Katika hatua nyingine Kafulila amesema anamtazama Lowassa kama kiongozi jasiri na mwenye malengo na uwezo wa kusimamia masuala hivyo kupitia Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) anaweza kufanya mambo makubwa zaidi kuliko angepitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) kama alivyotaka kufanya awali.
Mbali na hilo Kafulila amesema baada ya Uchaguzi Mkuu Mwezi Oktoba anaamini CCM itaunda kambi ya upinzani Bungeni kwa kuwa chama cha upinzani baada ya Ukawa kuchukua dola lakini pia anaamini kutakuwa na uwiano mzuri wa wabunge jambo ambalo kwa miaka mingi halikuwezekana.
"Bunge lijalo baada ya uchaguzi litakuwa bunge lenye uwiano mzuri wa wabunge wa chama tawala na watakaokuwa wapinzani, bila shaka CCM wataunda kambi rasmi ya upinzani," alisema Kafulila.
Jina la David Kafulila lilikuwa kubwa baada ya mbunge huyo kuibua bungeni kashfa ya akaunti ya Tegeta Ecsrow ambayo ilipelekea baadhi ya mawaziri kung'oka kwenye nyazifa zao na wengine kupelekwa katika tume ya maadili, lakini Mbunge huyo anayemaliza muda wake amesema baada ya kufichua uchafu huo wa serikali hana uhakika na usalama wake lakini amemkabidhi Mungu maisha yake.
"Baada ya kufichua skendo ya Escrow nilipata vitisho na nimendelea kupata vitisho, hakuna uhakika wa usalama na yote nimeshamkabidhi Mungu na nilikwenda kuhiji Israel mwaka jana," alisema Kafulila.
Kafulila alimaliza kwa kutoa maoni yake juu ya uchaguzi mkuu ambao unatarajiwa kufanyika Oktoba 25 na kusema kuwa utakuwa ni uchaguzi wa kihistoria kwa maana ya ukombozi wa awamu ya pili baada ya ule wa kumtoa mkoloni, na akakumbushia kauli ambayo baba wa taifa aliambiwa na wakoloni.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo