Familia moja ya watu watano eneo la Migombani
Tabata Segerea jijini Dar es Salaam imeugua ghafla baada ya kula tunda aina ya tikitimaji
linalosadikiwa kuwa na sumu
Baba wa familia hiyo Alphonce Kiduko akielezea
amesema baada ya kula tunda hilo hali ilianza kubadilika majira ya saa mbili
usiku na kila aliyekula alianza kuumwa tumbo la kuhara
Amesema hali hiyo ilianzia kwake na baadaye
kufuata kwa wanafamilia wengine ambapo baada ya muda wote walizidiwa na
kulazimika kumpigia simu daktari
Wanafamilia wengine waliofikwa na mkasa huo ni
Bariam Boniface na Anjelina Kiduko
Kwa upande wake muuguzi Blandina Charles
ameelezea hatua walizochukua kwa wagonjwa hao baada ya kupewa taarifa kuwa ni pamoja na kuwatundikia madripu pamoja na
kuwapa dawa za kunywa na mpaka sasa wanaendelea vizuri
Naye Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Migombani
Japhet Kemba amekiri kuwa na taarifa ya familia hiyo kufikwa na mkasa huo
