Na Ibrahim Mlele NJOMBE
Wakazi wa mtaa wa melinze Mjini Njombe wameshindwa kukubaliana na Mtendaji wao wa kata ya Mjimwema Bw Gerson Mbeyela juu ya mchango wa shilingi 1000 kwa mkazi wa kawaida na shilingi 3000 kwa mfanya biashara kumlipa mzabuni atakayekuwa akizoa taka katika vizimba vilivyopo ndani ya mtaa huo Licha ya kusema kuwa mzabuni huyo atatakiwa kuacha asilimia ishirini katika ofisi ya mtaa huo.
Hali hiyo imefikiwa baada ya wananchi kuhoji ni kwa nini mzabuni huyo ameshindwa kufika katika mkutano huo Ambaye Alitakiwa kufika ili aweze kutoa mchanganuo wa uchangiaji wa fedha hizo na namna gani zitatumika fedha hizo wakati wa kuondoa takataka katika mtaa huo.
Wakichangia katika mkutano huo Wamehoji nisheria ipi itatumika kumbana mzabuni asikimbie na fedha za wananchi Pindi Atakapochangisha Ambapo hata hivyo wananchi hao
wamesema kuwa ni lazima mzabuni anayefika awe makini katika kufanya kazi hiyo maana kuna baadhi ya wazabuni wanatelekeza kazi na kuwaacha wananchi wanaendelea kuumia kuchangia michango kwaajili ya kulipaa madeni hayo.
Kufuatia hali hiyo Mtendaji wa kata ya Mjimwema Bw Mbeyela Amelazimika kutolea maelezo juu ya kulipia kodi hiyo kwaajiri ya uzoaji wa taka Hizo Ambapo amesema kuwa mzabuni huyo hatakuwa tofauti na mzabuni wa mwanzo juu ya kuchangia katika uzoaji taka ndani ya mtaa huo.
Nao baadhi ya wafanyabiashara wa mtaa huo wamesema kuwa kuchangia shilingi 3000 kwao ni kiwango kikubwa Mno Huku Wakiitaka serikali kuwafikilia upya juu ya kiwango hicho Pamoja na kutazama upya juu ya kiwango wanachotoza na aina ya biashara wanayofanya.
Naye mwenyekiti wa Serikali ya mtaa huo Bw Erick John Msigwa amesema kuwa wao walimwandikia barua na kumfuata ili wapatiwe majibu ya kina juu suala la uzoaji wa taka na kusema kuwa mzabuni huyo alitakiwa kuwepo katika mkutano huo Jambo Ambalo Ameshindwa Kufika.
Nao baadhi ya wananchi waliohudhulia katika mkutano huo wamesema kuwa hawawezi kutoa hela ya taka mpaka mkurugenzi atakapofika katika mtaa huo ili aweze kuzungumza na wananchi wa mtaa ili waweze kufikia makubaliano juu ya suala la uzoaji wa taka katika mtaa huo.