Sasa Shilole "kupambana" na BASATA baada ya kumfungia

Huenda sasa Shilole anaweza kupata lepe la usingizi baada ya mwanasheria maarufu nchini, Albert Msando kuahidi kumsaidia kufuatia kupewa adhabu kali na baraza la sanaa la taifa, BASATA hivi karibuni.

BASATA lilimfungia muimbaji huyo wa ‘Nakomaa na Jiji’ kutojihusisha na sanaa kwa mwaka mzima kutokana na kitendo chake cha kuidhalilisha nchi alipokuwa akitumbuiza nchini Ubelgiji. Shishi amepost selfie Instagram akiwa na Msando na kuandika, “Nakuheshimu my kaka umeweza kujitoa kwa ajir yangu kwenye matatizo yangu! Mungu atakulipa inshaaalah @albertomsando.” 

Bongo5 imempigia simu Shilole kutaka kupata maelezo ya ni kwa vipi mwanasheria huyo anamsaidia lakini amedai kuwa yeye si mzungumzaji wa jambo hilo. Msando ni mwanasheria wa watu wengi mashuhuri akiwemo Zitto Kabwe. 

chanzo:bongo5 


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright 2025 EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo