Serikali kupitia idara ya uvuvi mkoa wa mara imekamata na kuteketeza kwa moto nyavu haramu za kuvulia samaki zenye thamani yazaidi ya shilingi milioni 98 baada ya kukutwa zitumika zikivua samaki ndani ya ziwa victoria kinyume cha Sheria.
Akizungumza kabla ya zoezi la uteketezaji wa nyavu hizo 3,285 kufanyika nje kidogo ya mji wa musoma,afisa mfawidhi wa usimamiziwa rasilimali za uvuvi kanda ya Mara Bw.Braison Meela,amesema nyavu hizo zimakamatwa katika operesheni inayoendelea baada ya kukutwa zikitumika kuvua samaki katika wilaya za Butiama, Bunda,Musoma na Rorya mkoani Mara.
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Musoma kamishina mwandamizi mstaafu wa jeshi la Polisi Zelothe Steven, pamoja na kupongeza juhudi hizo za kupambana na uvuvi huo haramu,lakini pia amataka operesheni hiyo kufanyika hadi katika maduka yanayouza nyavu hizo,huku mkurugenzi mstaafu wa taasisi ya utafiti wa uvuvi nchini Bw.Philip Bwathondi,akiwataka wanasiasa kuacha kufumbia macho uvuvi huo haramu.