Prof Peter Msolla "aliaga" jimbo la Kilolo Iringa

Na Matukiodaimablog Kilolo
ALIYEKUWA mbunge wa jimbo la Kilolo Prof. Peter Msolla (pichani juu) amekubali kushindwa katika kura za maoni na mkuu wa Wilaya ya Kaliuwa mkoani Tabora Bw. Venance Mwamoto Prof. Msolla akiwa mbele ya msimamizi mkuu wa uchaguzi aliyeagizwa na kamati kuu ya CCM Taifa , Luteni mstaafu Christopher Ngaleson na wajumbe wa kamati ya siasa ya Wilaya alisema kuwa amekubali kushindwa katika uchaguzi huo na kuyapokea matokeo hayo na kusaini.

Akitangaza matokeo hayo ya uchaguzi katibu wa CCM wilaya ya Kilolo Bw Clemence Mponzi alisema kuwa wagombea walikuwa 15 katika uchaguzi huo na Mwamoto alishinda kwa kura 13,713 huku akifuata Prof. Msolla kwa kupata kura 9,810 na nafasi ya tatu akifuata Danford Mbilinyi aliyepata kura 1,142.

Wakati chelestino Mofuga (576),Thadei Kikoti (136),Merick Luvinga (161),Anosta Nyamoga (68),Yefred Myenza (63),Luciana Mbosa (53),Francis Mkokwa(47),Mgabe Kihongosi (46),Ashraf Chusi (29) na Israel Salufu (9) 

Kwa upande wake Prof Msolla alisema kuwa amekubali ushindi wa Mwamoto na kuwa yupo tayari kuheshimu maamuzi ya kamati kuu ya CCM Taifa ” Nimekubali matokeo nipo tayari kufanya Kazi na atakayeteuliwa na chama Mimi kwangu chama kwanza mtu baadae” 

Huku Mgombea Francis Mkokwa mbali ya kumpongeza Mwamoto kwa ushindi huo bado alisema kuwa chama tawala kimeonyesha kumsikiliza Mgombea mmoja ambae alikuwa mbunge japo yeye ndie alicheza rafu katika michakato yote ya kura za maoni kwa kutaka kulazimisha matokeo.
Mkokwa alisema idadi ndogo ya wana CCM ndio walijitokeza kupiga kura kutokana na kuchukizwa na kurudia mara kwa mara zoezi hilo .
Hata hivyo Mkokwa aliwataka viongozi wa CCM ngazi za juu kuheshimu maamuzi ya wananchi katika kura za maoni kuliko kulazimisha kupita yule wanaemtaka wao kama walivyotaka kufanya katika jimbo hili 
Mshindi wa kura hizo za maoni jimbo la Kilolo Bw. Mwamoto aliwashukuru wana CCM Kilolo kwa kuonyesha Uwazi wao kwa mara zote uchaguzi uliporudiwa na kuwaomba radhi kwa kurudia uchaguzi huo huku akiwaomba wagombea wenzake kuunganisha nguvu ili kupata ushindi wa kishindo kwa Madiwani ,yeye kama mbunge na Rais Dr. John Magufuli

Mwamoto alipata kuwa mbunge wa jimbo la Kilolo mwaka 2000 hadi 2005 alipopokewa jimbo hilo na Prof Msolla ambae ameongoza kwa vipindi viwili sasa.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo