Aliyekuwa Mwenyekiti wa chama cha CUF taifa, Profesa Ibrahimu Lipumba akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na kung'atua rasmi umwenyekiti wa chama hicho na kuendelea kuwa mwanachama wakawaida wa chama hicho ikiwa atakuwa mwanachama halali kwani kadi yake ya uanachama ameshailipia mpaka mwaka 2020 hayo ameyasema katika ukumbi wa mikutano wa Peacock hoteli jijini Dar es Salaam leo.
Aliyekuwa Mwenyekiti wa chama cha CUF taifa, Profesa Ibrahimu Lipumba akiwa na wananchi wa kawaida kulia, Abdala Shabani pamoja na mdogo wake,Shabaani Miraji wakiwa wamemsindikiza aliyekuwa Mwenyekiti wa CUF taifa ili kuzungumza na waandishi wa habari kwa niaba ya wananchi katika mkutano uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa hoteli ya Peacock jijini Dar es Salaam leo.
Waandishi wa habari wakimsikiliza Aliyekuwa mwenyekiti wa chama cha CUFtaifa, Profesa Iblahimu Lipumba akitanga kujiuzulu wadhifa wake katika mkutano uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa hoteli ya Peacock jijini Dar es Salaam leo.
Aliyekuwa Mwenyekiti wa chama cha CUF taifa, Profesa Ibrahimu Lipumba akionyesha Rasimu ya Katiba pendekezwa ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania kuwa ndio iliyosababisha kuungana na kuunda umoja wa katiba ya wananchi (UKAWA) katika mkutano uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa hoteli ya Peacock jijini Dar es Salaam leo.
Aliyekuwa Mwenyekiti wa chama cha CUF taifa, Profesa Ibrahimu Lipumbaakionyesha Katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania ambayo katika mkutano wa kujivua uenyekiti wa chama cha CUF leo jijini Dar es Salaam.
Picha na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.