
Mzee Paul
Sozigwa (pichani), aliyewahi kuwa Mwandishi wa Habari wa Rais katika serikali ya Awamu ya kwanza
chini ya Mwalimu Nyerere, amepotea tangu jana mchana katika mazingira ya
kitatanishi.
Kwa mujibu wa taarifa ya familia yake ambayo Globu ya Jamii imeletewa, mara ya mwisho Mzee Sozigwa alionekana kanisani Mbezi Beach BCIC (kwa Gamanywa) jana
Alzheimer, na mara nyingi anapoteza kumbukumbu. Taarifa ya kupotea kwake
imeshatolewa polisi na kufunguliwa RB.
Taarifa hiyo imesema mara ya mwisho Mzee Sozigwa alikuwa amevaa shati
jeupe lenye mistari ya bluu na kijivujivu, suruali nyeusi na viatu vyeusi.
Anapoulizwa anakaa wapi hujibu Kisarawe ama Vidunda, wilaya ya Kisarawe.
Atakayemuona anaombwa kupiga simu zifuatazo:
Mch. Moses Sozigwa 0712 379818, 0755 716158
Mrs. Irene Yussuf 0784 300418
Ms. Lucy Paul Sozigwa 0755 564080, 0717 310783
Mrs. Judith Mlawa 0712 834737
Unaweza pia kuwasiliana nao kwa Whatsapp na
Viber