TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) taifa leo Agosti 17, 2015 katika kikao chake cha siku moja kilichofanyika katika Ofisi Ndogo za Makao Makuu ya CCM Lumumba jijini Dar es Salaa chini ya Mwenyekiti wa CCM Rais Dokta Jakaya Mrisho Kikwete imefanya uteuzi wa Wagombea Ubunge katika majimbo 9 kati ya 11 nchini yaliyokuwa yamebakia.
Wagombea Ubunge walioteuliwa na majimbo yao kwenye mabano ni:-
1. Ndugu Jerry Slaa - (Ukonga) Dar es Salaam
2. Ndugu Edward Mwalongo - (Njombe Kusini) Njombe
3. Ndugu Venance Mwamoto - (Kilolo) Iringa
4. Ndugu Raphael Chegeni - (Busega) Simiyu
5. Ndugu Edwin Ngonyani - (Namtumbo) Ruvuma
6. Ndugu Mohamed Mchengerwa - (Rufiji) Pwani
7. Ndugu Norman Sigara - (Makete) Njombe
8. Ndugu Martin Msuha - (Mbinga Vijijini) Ruvuma
9. Ndugu Joel Makanyanga Mwaka - (Chilonwa) Dodoma