Lowassa atua soko la Tandale jijini Dar

Wananachi wa maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam wamesema utaratibu wa mgombea urais wa Chadema kupitia UKAWA Mh Edward Lowassa wa kwenda kutembelea maeneo yenye kero ni dalili njema zinazoonyesha kuwa akiwa rais wa nchi hatadanganywa na watendaji walioko chini yake tatizo linalosababisha viongozi wengi kutoa maamuzi yasiyo sahihi na yanayoendelea kuiathiri jamii.

Wakizungumza baada ya Mh Lowassa na mgombea mwenza Mh Juma Haji Duni kutembelea masoko ya Tandale na Tandika jijini Dar es Salaam wananchi hao wamesema utaratibu huo ni miongoni mwa mambo yanayoonyesha tofauti na uwezo wa Mh Lowasa na wanasiasa wengine katika suala zima la uongozi, usimamizi na pia utatuzi wa kero za wananchi.
 
Katika hatua nyingine naibu katibu mkuu wachama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA Bw Salimu Mwalimu amesema baadhi ya changamoto ikiwemo ya malalamiko ya wagombea katika kata na majimbo zinaendelea kupatiwa ufumbuzi na kwamba uzinduzi rasmi wa kampeni za uchaguzi utafanyika jumamosi  29/08/15-katika viwanja  vya Jangwani.














JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo