Hali tete Simiyu, Fisi waendelea kutafuna na kuua watu

WAKAZI wengi wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi, mkoani Simiyu, wameingiwa na hofu baada ya kuwepo kwa matukio mfululizo ya watu kushambuliwa na fisi hadi kufa katika maeneo mbalimbali mjini hapa.
Matukio hayo yameelezwa kuendelea kutishia maisha ya wananchi katika wilaya hiyo, ambapo wengi wao walidai yanahusishwa na imani za kishirikina na kuiomba serikali kuchunguza kwa kina tatizo hilo.
Wakizungumza na waandishi wa habari katika tukio la kusikitisha la mwanamke ambaye hakutambuliwa jina wala anapoishi, kukutwa amekufa katika eneo la mtaa wa Kidinda, kata ya Bariadi baada ya kuvamiwa na fisi na kumsababishia mauti.
Katika eneo la tukio wananchi walisema kuwa hali kwa sasa katika mji huo imekuwa ya taharuki na hofu kutokana na kile walichodai kutokea kwa matukio hayo mara kwa mata. Walisema kwa nyakati tofauti kuwa katika kipindi cha mwezi, kumeripotiwa matukio manne ya aina hiyo.
“ Tunaishangaa ofisi ya maliasili wilaya hakuna, jambo ambalo wamelifanya wakati watu wanaendelea kupoteza maisha… Tunaomba waingilie kati. Angalia jamani ndugu zetu wanapoteza maisha, mbona zamani hawa fisi walikuwepo lakini hali hii haikuwepo? Ama si fisi wa kawaida hawa?” alihoji mkazi wa eneo hilo Elizabeth Mgema.
Akizungumzia hali hiyo pamoja na ofisi yake kulalamikiwa kutochukua hatua, Ofisa Maliasili wa halmashauri hiyo, Hellena Lintu alisema ofisi yake imeshindwa kutatua, hali hiyo kutokana na kutokuwa na uwezo wa kupambana na wanyama hao.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wilaya ambaye pia ni mkuu wa wilaya, Ponsiano Nyami, alithibitisha kupata taarifa za kuwepo kwa hali hiyo na kueleza kuwa tayari ameitisha kikao cha kamati ya ulinzi na usalama kuweka mikakati ya kupambana na wanyama hao


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo