Gari latumbukia mtoni na kuua watu 5 Njombe, Pia nyumba yachomwa moto kwa wivu wa kimapenzi


Na Gabriel Kilamlya, Njombe


Jeshi la Polisi Mkoani Njombe Limesema Limebaini Chanzo Cha Ajali ya Gari Iliyosababisha Vifo Vya Watu Watano Wilayani Ludewa Kuwa ni Mwendokasi Aliokuwa nao Dereva wa Gari Hilo.

Akizungumza na Vyombo Vya Habari Ofisini Kwake Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe Wilbroad Mutafungwa Amesema Kuwa Ajali Hiyo Iliyohusisha Gari Ndogo lenye Namba za Usajili T.613 AKA  Aina ya Toyota Cresta limeanguka Kwa Kutumbukia Katika Mto Baada ya Dereva Ambaye ni Aron Haule na Mmiliki wa Gari Hilo Kushindwa Kumudu Gari Kutokana na Mwendokasi Aliokuwa Nao na Kisha Kutumbukia Mtoni.

Kamanda Mutafungwa Amewataja Waliokufa Kuwa ni Pamoja na ARONI HAULE (40) , PENDO MBAWALA (29) , WESLAUS MTWEVE (40) ,EDITHA HAULE (35) na PASCALIUS MLWILO (20) ambaye ni mwanafunzi wa chuo cha Nursing Lugarawa.

Katika Tukio la Pili Kamanda Mutafungwa Amesema Jeshi la Polisi Mkoani Njombe Limepokea Taarifa kutoka Kwa 
Afisa Mtendaji wa Kijiji Cha Malembuli Kata ya Mang'oto Wilayani Makete bw. Alex Ponela Baada ya Kugundua Kuwepo Kwa Mauaji ya Joshua Salum Sudy Maarufu Kwa Jina la Mwaka Ambaye Amekufa Baada ya Nyumba Yake Kuchomwa Moto Kwa Wivu wa Kimapenzi.

Kufuatia tukio hilo kamanda ametoa Wito Kwa Watu Kuacha tabia ya Kujichukulia Sheria Mkononi na Kusababisha Madhara Makubwa ya Vifo na Uharibifu wa Mali Katika Maeneo Yao Jambo Ambalo ni Hatari Kwao kama walivyowanya katika kijiji cha Malembuli.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo