CUF yataja mwarobaini wa Prof. Lipumba


SIKU Chache kupita baada ya Profesa Ibrahimu Lipumba kutangaza kujiuzulu nafasi ya uwenyekiti ndani ya  Chama cha wananchi CUF, hatimaye Chama hicho kimeunda kamati ya muda itakayodumu kwa miezi sita ili kusimamia  nafasi za uongozi .
 
Hatua hiyo imetangazwa muda  mfupi  ulipita  jana Jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif ambaye ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wakati wa mkutano na waandishi wa Habari mara baada ya kumalizika Kikao cha Dharula cha Baaraza la kuu la uongozi wa chama hicho kilichoitishwa kujadili hatua hiyo ya kujiuzulu Profesa Lipumba .

Seif amesema katokana na Kanuni za CUF wamekubaliana kwa pamoja kuunda kamati maalum itakayosimamia chama kwa kipindi cha Miezi sita na baadae kufanya uchaguzi wa nafasi hiyo ya mwenyekiti.
 
Amesema Kamati hiyo itakuwa chini ya Katibu wa CUF ambaye ni yeye Maalim Seif na mwenyekiti wake atakuwa Mbunge wa Afrika Mashariki   Twaha Taslima na Kamati hiyo itakuwa na kazi ya kukijenga chama hicho,pamoja na kushirikiana na Vyama vyengine vinavyounda UKAWA  ambapo anadai itakuwa na jukumu lingine la  kuhakikisha wanaitoa CCM madarakani.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo