CHADEMA wakutana na kali ya mwaka wilayani Kyela

Na Ibrahim Yassin,Kyela

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wilayani Kyela Mbeya kimesikitishwa na kitendo cha wananchi kuziita Sakos Hospital za Serikali nchini kwa madai kuwa jina hilo linashusha hadhi,  mbali na kuwa baadhi ya hospitali za wilaya nchini hazina huduma rafiki kwa wananchi.

Akizungumza na wananchi jana kwenye mikutano ya hadhara wilayani humo,mwemyekiti wa baraza la vijana Chadema (BAVICHA) wilayani humo,Denis Maria,alisema baadhi ya wananchi wamekuwa wakiibatiza jina hospital ya wilaya kuwa ni sakos kutokana na kukosa huduma stahiki kwa wananchi.

Alisema wananchi wa Kyela asilimia 75 usafiri kwenda wilaya za Rungwe na Makete kufuata huduma bora za matibabu ambako nako kunaongezeko la fedha ya kumuona mganga isipokuwa dawa zinapatikana ikiwemo huduma nzuri ukilinganisha na Kyela.

Alisema kwa wilaya ya Rungwe gharama ya kumuona mganga imepanda kutoka elfu tatu hadi elfu nane ambapo watu bado wanamiminika kupata huduma kwenye hospitali hiyo inayodaiwa kuwa inaunafuu kwa upatikanaji wa dawa na vifaa tiba.

Maria akizungumza huku mamia ya wananchi wakipiga makofi akisisitiza kuwa endapo Ukawa watafanikiwa kuchukua nchi watabadirisha mfumo huo ambao amedai ni kandamizi kwa wananchi na kuweka huduma bora kwa utaratibu mzuri utakao muondolea kero mwananchi.

Mkatibu wa Siasa na uenezi wilayani humo,Donald Mwaisango,alisema wakishika dora oktoba 25 mwaka huu watahamasisha wananchi kijiunga na mfuko wa bima ya Afya na kuwawezesha wasiokuwa na uwezo kupata bima pamoja na kuboresha huduma za afya ili wananchi wajenge imani na hospital yao.

blog hii ilibisha hodi kwa mganga  mkuu wa wilaya ya Rungwe Dkt,Sungwa Ndagambwa ambaye alikiri ongezeko hilo na kusema hospitali yake imekuwa ikihudumia wananchi kutoka wilaya za jirani ambapo wameongeza gharama hiyo ili waweze kumudu gharama za kuleta dawa kwa wingi.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo