CCM wasema hawashtushwi na makada na viongozi wanaoendelea kuhama na kujiunga na CHADEMA

Chama cha mapinduzi kimesema hakishtushwi na makada na viongozi wanaoendelea kukihama chama hicho na kujiunga na Chadema na kudai kuwa wanao ondoka wana sababu zao binafsi na kwamba hakuna kiongozi wa upinzani ambaye hakuanzia CCM hivyo ni hali ya kawaida kwa chama kikubwa kama hicho ambacho kina mtaji wa wanachama takribani milioni nane.

Katibu wa NEC, itikadi na uenezi wa CCM, Bw Nape Nnauye, amebainisha hayo wakati akitoa ufafanuazi wa masuala mbalimbali yanayokihusu chama hicho kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam ambapo amesema waliohama na watakaoendelea kuhama siyo jambo jipya kwani kuna viongozi wakubwa waliondoka huku akitolea mfano wa Maalim Seif na Agustino Mrema.

Akizungumzia suala la changamoto zinazoibuka katika kura za maoni zinazoendelea katika baadhi ya majimbo na kusema kuwa zinafanyiwa kazi katika ngazi husika kabla ya kufikishwa ngazi ya taifa na kuwataka wafuate taratibu na kwamba majimbo ambayo kura za maoni zinarudiwa, matokeo yake yatatangazwa baada ya kupitishwa na kamati kuu ya chama hicho Agosti 17 mwaka huu.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo