KATIBU wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Iringa, Hassan Mtenga amewaambia wajumbe wa halmashauri ya CCM Manispaa ya Iringa kwamba ushindi wa CCM katika uchaguzi mkuu ujao hauwezi kupatikana kwa kupiga nyimbo za TOT.
“Hatuwezi kushinda kwa kusikiliza nyimbo za Komba, ni lazima tufanye kazi ya siasa,” alisema wakati akiwakabidhi msaada wa vipaza sauti vyenye thamani ya Sh Milioni 36.
Pamoja na kuahidi kumpiga chini Mchungaji Peter Msigwa katika uchaguzi huo, Mtenga alisema kazi kubwa iliyoko mbele yao ni kukutana na wapiga kura zaidi ya 100,000 wa jimbo la Iringa Mjini.
“Tuwaeleze kwanini wanatakiwa kuendelea kuimani CCM na kuichagua na kwanini hawatakiwi kumchagua Msigwa na Ukawa yao,” alisema.