Breaking News: Waziri Binilith Mahenge aanguka kura za maoni Makete

Prof. Norman Sigalla.
Na Eddy Blog Makete

Matokeo ya kurudiwa kwa uchaguzi wa kura za maoni jimbo la Makete kupitia chama cha mapinduzi CCM yamekamilika na kutangazwa rasmi kwa wananchi

Hatua ya kurudiwa uchaguzi huo uliofanyika jana iliamuliwa na vikao halali vya Chama cha mapinduzi vilivyoketi wiki hii mkoani Dodoma na kuamua uchaguzi huo urudiwe baada ya matokeo ya awali kutoridhisha baadhi ya wagombea hivyo kukawepo na rufaa

Akitangaza matokeo hayo leo Mkurugenzi wa uchaguzi huo ambaye pia ni katibu wa CCM wilaya ya Wanging'ombe na kaimu katibu wa CCM wilaya ya Makete Bw. Jumanne Kapinga amesema Prof. Norman Sigalla amepata kura 8838, akifuatiwa na Dkt Binilith Mahenge aliyekuwa akitetea nafasi yake na kupata kura 7885, Bonike Mhama 124, Fabian Nkimwa 74 na Lufunyo Nkinda 42

Kwa mantiki hiyo amemtangaza mshindi wa uchaguzi huo kuwa ni Prof. Norman Sigalla ambaye atapeperusha bendera ya chama hicho katika uchaguzi mkuu wa Mwaka huu kwa jimbo la Makete

Awali katika kura za maoni za mwanzo za Agosti Mosi mwaka huu, Dk Mahenge aliongoza kupata kura 8,534 huku Profesa Sigalla akipata 8,211, Mhami (500), Nkimwa (486) na Nkinda (226).
Kwa kile kilichothibitisha kuwepo kwa udanganyifu wa matokeo ya awali, baadhi ya wana CCM wa jimbo hilo walilazimika kusafiri hadi makao makuu ya CCM ya wilaya ya Mahenge, kupinga matokeo hayo.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo