Bibi ageuka "dili" wakati wa mapokezi ya Lowassa jijini Mbeya

Katika hali ya Kushangaza  Kamera ya Mbeya yetu iliwanasa vijana wapatao kama saba wakiwa na Bibi kizee ambaye hakutambulika kwa majina, vijana hao walionekana kumtengeneza Bibi kwa ajili ya kupata kipato kwa mtu yoyote kutoa chochote ili kupiga Picha na Bibi huyo. vijana hao walionekana wakali kuona kama watu wanapiga nae picha bila kutoa chochote ... Tukio likawa hivi...
 Huyu ndiye Bibi ambaye jina lake halikufahamika mara Moja, Hapa akiwa anapigwa pica na mtu ambaye alichangiwa.. Mtandao huu ulishuhudia akipewa maelekezo ya nini afanye Bibi huyo ikiwa ni pamoja na kunyoosha vidole juu.
 Hawa ni Baadhi ya vijana ambao wao ndio walikuwa wakitoa maelekezo kwa Bibi nini cha kufanya pindi anapotakiwa piga picha na wananchi ambao walitakiwa kuchangia kabla ya Kupata ukodaki huo na Bibi.. ambapo bibi  huyo alifuata tu maelekezo ya vijana hao
 Kamera yetu iliendelea kufuatilia hatua kwa hatua na kuona vijana hao wakiendelea kumtembeza Bibi huyo na kuendelea kupata kipato Buree...

 Hapa Bibi huyo akiwa ameshikiria kitita cha Fedha ambazo alikusanya kutoka kwa waliopiga picha nae, na ili upige Picha zote ilikuwa ni lazima uchangie kitu..

Mpaka tunaondoka eneo la Tukio Bado vijana walikuwa wanaendelea  kupata kipato...

Picha na Mbeya yetu 


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo