Auawa alipokuwa akijaribu kumwokoa mwanafunzi mwenzake asibakwe

Mwanafunzi wa kidato cha pili wa Sekondari ya Nyasubi Shinyanga, Ally Jacob ameuawa baada kuchomwa na kitu chenye ncha kali shingoni alipokuwa akijaribu kumwokoa mwanafunzi mwenzake asibakwe.
Tukio hilo lilitokea wakati mwanafunzi huyo alipokuwa akirejea nyumbani kutokea shuleni… 
Kamanda wa Polisi Shinyanga, Justus Kamugisha alidai kuwa mwanafunzi huyo aliuawa kwa kuchomwa na kitu chenye ncha kali sehemu ya shingoni na mwenzake anayesoma Sekondari ya Kishimba.
Kamugisha alisema sababu za Jacob kuuawa ni kujaribu kumsaidia mwanafunzi mwenzake mwenye umri wa miaka 16 ambaye anasoma kidato cha pili Sekondari ya Nyasubi ili asibakwe na mtuhumiwa ambaye alitaka kufanya unyama huo kwa kushirikiana na mkazi mmoja wa Nyasubi.
Alisema watuhumiwa wote wamekamatwa na watafikishwa mahakamani baada ya upelelezi kukamilika.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo