Waziri aukosa Ubunge viti maalum mkoa wa Njombe

NAIBU Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Dk Pindi Chana amepigwa chini katika kura za maoni za ubunge wa viti maalumu kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Njombe.

Wajumbe wa mkutano wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) wa chama hicho, mkoania Njombe walimchagua Dk Suzan Kolimba na Neema Mgaya kuingia katika kundi la washindi wawili wa ubunge wa viti maalumu kutoka kila mkoa nchini katika kura za maoni zilizofanyika jana, mjini Njombe.

Wakati Dk Kolimba alikuwa mshindi wa kwanza kwa kupata kura 252, Mgaya alikuwa wa pili akipata kura 213 huku Dk Chana akiambaulia kura 164 zilizofanya awe mshindi wa tatu, ushindi ambao haumpeleki tena bungeni kuwakilisha wanawake wa mkoa huo.

Mwingine aliyeanguka katika kura hizo za maoni ni Mkuu wa Wilaya ya Ileje, Rosemary Sitaki aliyeambulia kura 38 huku Erika Sanga akipata kura 107 na Magret Kyando akiambulia kura tano.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright 2025 EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo