Uchaguzi wa CHADEMA Karatu majibu yao hapa

Kinyany’anyiro cha ubunge kupitia tiketi ya chama cha CHADEMA kimemalizika katika wilaya ya karatu huku William Kumbala akiibuka mshindi kwa kura mia mbili kumi na saba dhidi ya wagombea wengine na mbunge wa zamani mchungaji Israel Natse akidai ameacha ubunge wa hiari yake baada ya kanisa kumtaka arudi katika uchungaji ili kuhudumia jamii katika roho.

Wakizungumza baada ya kumalizika kwa uchaguzi huo mwenyekiti wa CHADEMA kanda ya kaskazini  mchungaji Israel Natse amesema katika kipindi hiki kila chama kinatakiwa kusimamisha mgombea mwadilifu anayechukua rushwa na harufu ya ufisadi hivyo anahitaji mrithi makini kama ilivyo kuwa yeye ambaye ameachia kijiti kwa hiari yake.
 
Kwa upande wake mbunge wa Arumeru Mashariki Joshua Nasari amesema watanzania wamekiamini CHADEMA kwa kuwa kimeonesha kutetea wananchi na kukemea matendo maovu hivyo lazima kiongozi anaye toka chadema awe msafi asiye na sifa za kuhujumu mali za wanachi huku katibu wa CHADEMA mkoa wa Arusha Calist Lazaro akielezea jimbo la karatu kuwa ni jimbo la mfano katika mageuzi ya kweli hapa nchini.
 
Katika uchaguzi huo uliyo shirikisha wagombea watano Bwana William Kumbala ameibuka mshindi kwa kura miambili na kumi na saba na kuwabwaga wagombea wengine wanne akiwemo aliyekuwa mwenyekiti wa halmashauri ya Karatu Lazaro Maasai.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright 2025 EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo