
Mwezi uliyopita Serikali ya South Africa ilifanya mabadiliko ya Sheria hiyo na Mwenyekiti wa Kamati Kwingineko juu ya Haki na Huduma za Magereza Mathole Motshekgaalisema hapo awali aliamini kuwa kama jamii jukumu lao ni kuwafundisha watoto kujichunga, lakini alikuwa anakosea na kuwanyima watu hao haki zao za kibinadamu.
Bunge la Katiba lilikaa na kufanya mabadiliko juu ya vifungu 15 na 16 ya Sheria hiyo kwa kusema kuwa Vifungu hivyo vinaenda kinyume na Katiba inayosema kila Raia ana uhuru wa maamzi yake binafsi na pia ni kinyume na haki za binadamu.
Bunge la Katiba limesema kila mtu iwe mkubwa au mdogo ana haki ya kufanya maamuzi binafsi yanayomhusu yeye bila kupingwa au kuingiliwa na mtu yoyote.