Wala chakula chenye sumu katika sherehe mkoani Dodoma

Watu saba wamenusurika kifo baada ya kula chakula kinachodaiwa kuwa na sumu kwenye tafrija ya maulidi ya kumtoa mtoto nje katika eneo la Nkuhungu manispaa ya Dodoma.

Watu hao mara baada ya kula chakula hicho ambacho kilikuwa ni kitoweo cha nyama ya mbuzi mikate na asali walianza kutapika mfululizo kabla ya wasamaria wema kuwakimbiza hosipitali ya rufaa ya mkoa wa Dodoma ambapo muuguzi mfawizi wa hosipitali hiyo Rehema Mghina akithibitisha kupokea watu hao huku akisema kuwa bado wako kwenye utafiti wa kitabibu ili kugundua wagonjwa hao wanasumbuliwa na tatizo gani.
 
Hata hiyo watu hao baada ya kulazwa kwa zaidi ya masaa 24 wameruhusiwa kurudi majumbani ambapo wameeleza kilicho wasibu mara baada ya kula chakula hicho huku waandaaji wa sherehe hiyo wakibaki na sitofahamu kuhusu tukio hilo.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo