Zaidi ya wafanaykazi 200 wa kampuni ya Bim International inayojenga uwanja wa ndege wa kimataifa maarufu kama Terminal 3 jijini Dar es Salaam wamegoma kufanya kazi kufuatia uongozi wa kampuni kushindwa kutatua madai yao ambayo ni ya muda mrefu.
Wanasema tunataka haki zetu, miongoni mwa haki hizo wanazodai waajili hawa wa kampuni ya Bim International ya Uholanzi inayojenga uwanja wa ndege wa Terminal 3, ni pamoja na dai la kuongezewa mishahara, kodi ya nyumba, kutokuwa na imani na uongozi wa kampuni hiyo, adhabu za mara kwa mara zinazofanya wengi wao kuachishwa kazi kila kukicha, wanadai licha ya kuomba fursa ya kuzungumza na uongozi wa kampuni hiyo Bim Internatinal maombi hayo yamekuwa yakifikishwa na moja ya maafisa wa chama cha wafanyakazi kutoka TAMCO.
Utofauti wa malipo ya sh 65000 kwa Sub Contractors na malipo ya sh 30000 kwa wafanyakazi wa kampuni mama ya Bim International ambapo jitihada za kuonanana na maafisa wa kampuni hiyo ziligonga mwamba Na hata hivyo bado tunawatafuta kuzungumzia sakata hilo.
