Mwenyekiti wa Kampeni iliyolenga kupata fedha kwa ajili ya kuwasaidia wanahabari wanaougua magonjwa sugu yakiwepo ya saratani, (MEDIA CAR WASH FOR CANCER) , Benjamin Thompson akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kutangaza kiasi cha fedha kilichopatikana katika harambee ya jijini Dar es Salaam ambapo kiasi cha shilingi Milioni 31 zilipatikan ikiwa ni ahadi na taslimu. Kulia ni Mjumbe wa Kamati hiyo ambaye pia ni Mkurugenzi Msaidizi wa MAELEZO, Zamaradi Kawawa. Harambee nyingine kama hiyo inataraji kufanyika Jijini Mwanza mwezi Agosti mwaka huu.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Dar es Salaam Julai 9, 2015
JUMLA ya
shilingi milioni 31 zimepatikana katika harambee ya kuosha magari iliyofanywa
na waandishi wa habari Julai 4, 2015 katika viwanja vya Leaders Club, Jijini
Dar es Salaam. Kati ya fedha hizo, taslimu ni Milioni 12 na zingine ni ahadi.
Harambee
hiyo inajulikana kwa jina la Media Car Wash for Cancer. Lengo la changizo hilo
lilikuwa kupata Shilinngi Milioni 100, ili kuwahudumia waandishi wenye matatizo
mbalimbali ya kiafya pamoja na kuwaingiza waandishi wa habari kwenye mfumo
rasmi Bima ya Afya.
Kama tulivyotanzaga awali, wagonjwa ambao ni
walengwa Adolf Simon Kivamo, Dastan
Bahai na Athumani Hamisi.
Ili
kutimiza lengo la changizo, Kamati ya Media Car Wash for Cancer inatarajia
kuendelea na zoezi la kutafuta pesa mpaka kiwango hicho kitakapofanikiwa.
Mpaka sasa
Kamati imeweza kuunda kamati ndogondogo zitakazosimamia zoezi la ufuatiliaji na
ukusanyaji fedha kulingana na ahadi mbalimbali na wataifanya kazi hiyo kwa muda
wa wiki moja.
Kisha,
wajumbe wa kamati hii ambayo jumla yao ni 75 watatoa maamuzi wa mgao huo mara
moja.
Kamati
hizo pia zitafanya kazi ya kuwatambua idadi ya kamili ya waandishi wengine
wanaosumbuliwa na magonjwa mbalimbali na hawana msaada unaoeleweka.
Aidha, hali
kadhalika, kamati hiyo pia inafanya tathimini ili kujua idadi ya wanahabari
ambao hawana Bima ya Afya ili utaratibu wa kuwaingiza kwenye mpango huo
uandaliwe.
Katika
awamu hii ya kwanza tunatarajia kuanza na wanahabari 50 ambao sio waajiriwa,
lakini wanafanya kazi katika vyombo vya habari nchini yaani correspondents.
Uteuzi wa
majina ya waandishi utakwenda kwa kufuatana, yaani kutoka na chombo kimoja hadi
kingine.
Hii ni
mara ya kwanza katika historia ya Tanzania kwa waandishi wa Habari kuwa na
mfuko huu ambao lengo lake ni kwasaidia katika masuala ya matibabu.
Kamati itaanza
na waandishi wa habari walioko kwenye vyombo vya habari vya Jijini Dar es
Salaam na baadaye kuendelea katika mikoa mingine nchini.
Aidha,
Kamati ya Maandalizi ya Harambee hii imeitisha mkutano mkuu wa wadau wa habari
nchini utakaofanyika alhamisi Julai 16, 2015 kwa ajili ya kuanzisha mchakato wa
usajili wa chombo hiki muhimu.
Wahariri
wenu watakujulisheni muda na mahali utakapofanyika mkutano huu.
Pia,
kamati hii inakusudia kufanya harambee nyingine katikati ya mwezi Agosti mwaka
huu, itakayofanyika Jijini Mwanza.
Hatua za
awali za harambee hiyo kwa kushirikiana na wenzetu wa Jiji hilo zimeanza,ikiwa
ni pamoja na kutafuta eneo la kufanyia shughuli hiyo pamoja na wadhamini
mbalimbali.
Mwisho
tungependa kutoa shukrani zetu za dhati kwa wadhamini na wadau wote
walioshirikiana nasi katika harambee hii ambao ni BOT,TPB, NHIF, TANAPA, NSSF,
JUBILEE INSURANCE, ANSAF, ASTE INSURANCE, MOIL,TAGCO,TEA, Wizara Ya Habari,
Vijana, Utamaduni na Michezo,Bw. Reginald Mengi, Mh.Hamis Kagasheki, Mh.
Ridhiwani kikwete, Mh.Shabiby, Clouds FM, Radio Five,New Habari. The Guardian
Ltd, pamoja na Wanakamati,
Benjamin
Andongolile Thompson
Mwenyekiti
wa Kamati ya Maandalizi
Media
Campaign for Cancer Campaign
