Uchakavu wa majengo wahatarisha uhai wa wanafunzi huko Monduli, Angalia hapa


 Jengo la shule ya msingi Donyonaado.

 Na Woinde Shizza,Monduli
Wakati shule nyingi nchini zinafunguliwa baada kumalizika kwa likizo Wanakijiji wa kijiji cha Donyonaado kilichopo wilaya ya Monduli mkoani Arusha wameeleza wasi wasi juu ya uchakavu wa jengo la shule ya Msingi 
Idonyonaado huenda linaweza kuanguka na kusababisha maafa kwa 
wanafunzi.

 Shule hiyo iliyoko umbali wa kilomita 64  kutoka Monduli mjini 
iliyojengwa kwa udongo na mawe na wanakijiji waliojitoa haina milango 
na madirisha hivyo wanafunzi kupata adha ya vumbi na baridi  kali hasa 
kipindi cha mvua.

 Wanakijiji hao wamesema kuwa  hali mbaya  ya miundombinu ya shule hiyo 
imewafanya wazazi wengi kusita  kuwapeleka watoto mashuleni  hivyo 
ameiomba serikali na mashirika binafsi yajitokeze kusaidia kutatua 
changamoto hizo.

 Mwenyekiti wa kijiji cha Donyonaado ,Malulu Kutetei amesema kuwa licha 
ya changamoto za shule hiyo bado wanakabiliwa na tatizo la ukosefu wa 
nyumba bora za walimu pamoja na uhaba wa maji jambo linalokwamisha 
maendeleo ya taaluma shuni hapo.

 Mkurugenzi wa Shirika lisilokuwa la kiserikali la Wafugaji la Monduli 
Pastodalist Development Initiative (MPDI) ,Erasto Sanare ameeleza 
kusikitishwa na changamoto zinazoikabili shule hiyo hivyo kushiriki 
katika  ujenzi wa shule ya kudumu ,ameieomba serikali isaidia shule 
hiyo ambayo ni tegemeo kwa wafugaji.

 Licha ya Jamii ya Wafugaji kuamka katika masuala ya elimu tofauti na 
miaka iliyopita bado kuna mazingira duni ya elimu ikiwemo kukosekana 
kwa shule za kutosha,miundombinu mibovu,uhaba wa maji na vifaa vya 
kufundishia na nyumba za walimu


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright 2025 EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo