Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imesogeza mbele muda wa kuanza zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura katika mkoa wa Dar es salaam ambalo lilipangwa kuanza tarehe 16/07/2015, ambapo sasa litanza tarehe 22/07/2015.
Kwa mujibu mwenyekiti wa NEC, Jaji Mstaafu Damian Lubuva uamuzi huo umefikiwa baada ya kuridhia maombi ya wadau wa uchaguzi kusogezwa mbele siku ya kuanza zoezi hilo ili kutoa fursa kwa wananchi kusherehekea Siku Kuu ya Eid-El-Fitri.