Madereva mabasi, malori na daladala hapa nchini wameazimia kusitisha kuendesha magari nchi nzima endapo kamati iliyoundwa kwa ajili ya kutetea maslahi yao haitatoa majibu ya haraka kuhusu kuanza kutumika kwa mkataba baada ya kupitiwa na kujadiliwa kwa rasimu ya mkataba huo ambayo wamekiri kuridhika nayo.
Naibu Katibu Mkuu wa chama cha Wafanyakazi Madereva Tanzania Rashid Saleh ambapo amebainisha kwamba iwapo hakutakuwa na tamko lolote wiki hii kutoka kwa kamati hiyo, basi wiki ijayo siku isiyojulikana madereva hao watagoma mpaka makubaliano yaliyofikiwa yatekelezwe.
Aidha, Naibu Katibu Mkuu huyo amesema kinachokwamisha ni kwa wizara ya kazi kuendele kuchelewesha kutangaza tarehe rasmi ya kuanza kutumka kwa mikataba hiyo.
Mgogoro kati ya chama cha wafanyakazi madereva Tanzania, wamiliki wa magari na serikali ulimalizwa na mkuu wa wilaya ya kinondoni baada ya makubalianao kadhaa ikiwemo kuwapatia haki zao za msingi madereva hao hususan mikataba ambayo mpaka leo haijulikani lini itaanza kutumika.